Sema na Mahakama ni mfumo wa kutuma na kupokea malalamiko pamoja na Maulizo kutoka kwa wananchi.
Ndio, unaweza kutuma lalamiko lako kwenye Mahakama husika.
Ili uweze kutuma lalamiko unatakiwa kuwa na simu ya mkononi (smartphone) / kompyuta / kishikwambi (tablet).
Unaweza kutuma lalamiko wakati wowote na mahali popote ila tu unatakiwa kuwa na mtandao mzuri.
Ndio, unachotakiwa kufanya ni kubofya msimbo (*152*00#) kisha utachagua tuma lalamiko.
Unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye tovuti ya Sema na mahakama (https://sema.judiciary.go.tz/), bonyeza sehemu iliyoandikwa Sema na Mahakama App, pakua, na sanikisha (install) kwenye simu yako.
Ndio, unaweza kutumia Mobile App au tovuti kufungua akaunti yako ya Sema na mahakama unachotakiwa ni kujaza taaarifa zako kwa usahihi ili uweze kupata mrejesho wa pale unapotuma lalamiko lako.
Hapana, huduma hii ni bure kabisa unachotakiwa ni kuwa na namba ya simu kwaajili ya kupata namba na mrejesho wa lalamiko lako.
Ndio, unaweza kutuma lalamiko bila kujulikana unachotakiwa ni kuchagua sehemu ya tuma lalamiko bila kujulikana kwenye tovuti au Mobile App.
Kuna njia 2 (mbili) za kujua lalamiko lako limepokelewa na kujibiwa au la!
a) Kwanza kwa kutumiwa ujumbe mfupi kupitia simu yako ya mkononi endapo ulitumia akaunti yako ya sema na mahakama / ulijaza taarifa zako / Msimbo.
b) Pili kwa kutumia Namba (ID) ya lalamiko kupitia tovuti ya Sema na mahakama, Mobile App au Msimbo.